PHARMACEUTICAL SCIENCES

Idara ya Ufamasia - Kolandoto College

Maelezo Kuhusu Kozi

Fani ya Ufamasia / Madawa

Ufamasia ni fani ya afya inayojikita katika ugavi, utayarishaji, utoaji, na usimamizi wa dawa. Wataalamu katika fani hii wanajulikana kama mafamasia au wafamasia. Kazi yao kuu ni kuhakikisha matumizi sahihi na salama ya dawa kwa wagonjwa, pamoja na kutoa ushauri na elimu kuhusu matumizi ya dawa hizo.

Wafamasia kwa ufupi tunasema ni wale wanaokupatia dawa hospitali pale unapoambiwa na daktari nenda kwenye dirisha la dawa au hata katika maduka ya dawa. Kutoa dawa ni kazi moja na huwenda ndiyo ndogo kabisa kwa taaluma hii. Taaluma yao huwawezesha pia kutengeneza dawa, kuchanganya dawa, kusimamia uhifadhi na usambazaji wa dawa pia.

Majukumu ya Mfamasia

  1. Kutoa Dawa: Mafamasia wanahusika na utoaji wa dawa zilizoandikiwa na madaktari. Wanazingatia dozi sahihi, njia za matumizi, na muda wa matumizi wa dawa hizo.
  2. Elimu ya Afya: Wanatoa elimu kwa wagonjwa na umma kwa ujumla kuhusu matumizi sahihi ya dawa, athari za dawa, na jinsi ya kudhibiti madhara yanayoweza kutokea.
  3. Usimamizi wa Dawa: Mafamasia wanahakikisha kuwa dawa zimehifadhiwa vizuri, na kwamba hazijaisha muda wake wa matumizi. Pia wanahusika na upatikanaji wa dawa bora na zenye ubora wa juu.
  4. Utafiti na Maendeleo: Wana jukumu la kufanya utafiti kuhusu dawa mpya, pamoja na kuendeleza njia mpya za tiba. Hii inajumuisha majaribio ya kliniki na ushirikiano na wanasayansi wengine.
  5. Huduma za Kliniki: Katika baadhi ya maeneo, mafamasia wanashiriki moja kwa moja katika kutoa huduma za kliniki kama vile kuchukua vipimo vya afya, kutoa chanjo, na kushauri kuhusu magonjwa mbalimbali.

Elimu na Mafunzo

Mafunzo haya yanajumuisha masomo ya kemia, biolojia, fiziolojia, na sayansi ya dawa. Baada ya kumaliza masomo ya darasani, wanafunzi pia hufanya mafunzo kwa vitendo katika hospitali, maduka ya dawa, na viwanda vya dawa.

Fursa za Kazi

  1. Maduka ya Dawa: Hii ndiyo sehemu kubwa ambapo mafamasia hufanya kazi, wakitoa dawa na ushauri kwa wagonjwa.
  2. Hospitali: Mafamasia wa hospitali wanashirikiana na madaktari na wauguzi katika kutoa huduma za tiba kwa wagonjwa waliolazwa na wanaohudhuria kliniki.
  3. Viwanda vya Dawa: Mafamasia wanahusika na utafiti, maendeleo, na uzalishaji wa dawa mpya. Wanashiriki katika majaribio ya kliniki na kuhakikisha ubora wa bidhaa za dawa.
  4. Elimu na Utafiti: Mafamasia pia wanaweza kufanya kazi kama wakufunzi katika vyuo vikuu na taasisi za elimu ya juu, wakifundisha wanafunzi wa ufamasia na kufanya utafiti katika maeneo mbalimbali ya sayansi ya afya.
  5. Mashirika ya Serikali na Udhibiti: Wanashiriki katika udhibiti wa ubora wa dawa, kuhakikisha kuwa sheria na kanuni za dawa zinafuatwa, na kufanya kazi katika mashirika ya udhibiti wa dawa na chakula.

Vigezo vya Kujiunga

Walio na Mtihani wa Cheti cha Elimu ya Sekondari (CSEE) wenye ufaulu (Alama D) wa masomo manne (4) yasiyo ya kidini ikiwemo Kemia, Biolojia na Fizikia. Kama una Ufaulu katika Hisabati na Lugha ya Kiingereza unajiongezea nafasi zaidi.

Pharmacy Image

Ada na Michango

Kolandoto College of Health Sciences

Tuition Fee and Other Contributions for Academic Year 2023/2024

Department of Pharmaceutical Sciences

No Detail Semester 1 Semester 2 Total Payment
1 Tuition Fee 1,000,000.00 600,000.00 1,600,000.00
Other Contributions
2 Internal Examinations 200,000.00 150,000.00 350,000.00
3 Accommodation 150,000.00 150,000.00 300,000.00
4 Library Services 25,000.00 25,000.00 50,000.00
5 College Development 50,000.00 50,000.00 100,000.00
Total Payment per Semester 1,450,000.00 1,000,000.00 2,450,000.00

NB: Mwanza saa za kazi: 8:00 AM hadi 10:00 AM.

Fomu ya Kujiunga

Registration Form for the Year 2024-2025

Mawasiliano ya Idara

Wasiliana nasi kwa simu: +255 757 164 416
Au kwa namba ya pili: +255 620 339 260